2: chagua
Katika kila shilingi
unayopata na kuishika mkononi una uhuru wa kuchagua mstakabali wako wa kuwa
tajiri au masikini au mtu wa daraja la kati. Namna yako ya matumizi inaeleza
wazi wazi wewe ni mtu wa namana gani. Kwa hiyo katika wakati huu ulio nao
chagua kuwa tajiri. Na ukitaka kuwa tajiri jifunze namana ya kumiliki mali,
mali ya kweli na sio ya kupita. Vijana wengi hurithi mali kutoka kwa wazazi wao
na huipoteza bila kujua kwasababu hawajifunzi namna ya kuitunza, hivyo hata
tukirithi mali bado tuna jukumu la kujifunza namna ya kuitunza na kuifanya iwe
mali ya kweli.
Watu wengi huchagua kubaki
masikini kutokana na kuwa na imani mbalimbali wengine husema “mimi sipendi
hela”, “hamna shida mimi bado kijana bado nina muda”, “nikipata hela ya kutosha
ndio nitafikiria nini cha kufanya”, “hamna shida mbona baba yangu ana fedha ya
kutosha”. Mawazo kama hayo yanamfanya mtu afikie upeo wake wa kufikiri. Hata
kama huna fedha jifunze juu ya kuzimiliki. Lakini bado tunabaki na uamuzi wa
kuchagua kila siku; nini cha kufanya na muda wetu,fedha zetu,na nini cha kuwaza
katika vichwa vyetu chaguo liko juu yetu. Na huo ndio uhuru wa kuchagua uhuru
ambao kila mtu anao na ana wajibu wa kuutumia, uhuru wa kuchagua kuwa tajiri na
tuna takiwa kuchagua kuwa matajiri kila siku ya maisha yetu.
WEKEZA KATIKA ELIMU;
Hakuna mtu anayeweza
kukunyang’anya akili. Akili ndio mali pekee ambayo binadamu amejaliwa. Kila mtu
ana uhuru wa kuchagua nini cha kuweka katika ubongo wake mala tu anapokuwa mtu
mzima. Nyingi kati ya biashara zetu hufa kwasababu tunazianzisha kabla ya
kujifunza namna ya kuendesha biashara. Hata leo hii naaandika kitabu
kinachogusa maisha yetu ya kila siku lakini sijui ni watu wangapi watakihitaji
na kukinunua badala ya kutumia fedha zao kununua pombe na CD za muziki na
filamu. Wengi wetu tumeishia kununua TV na VCR,VCD, DVD n.k na ni wachache sana
wanaonunua vitabu. Huo ndio uhuru wa kuchagua, ambao unabaki mikononi mwa kila
mtu binafsi.
3: marafiki
Ushirikiano ndio nguzo ya
mafanikio, utafanya ushirikiano na nani?. Hakika jibu litakuwa ni marafiki, ONYO, chagua marafiki na wala usiwachague
kutokana na uwezo walio nao kiuchumi. Tuwe na marafiki, wawe mamilionea au
mafukara nia hasa ni kujifunza kutoka kwao wote tena kwa ufahamu wa hali ya
juu.
Namna yetu ya kujumuika na
marafiki tajiri iwe ya makini wasije wakahisi kuwa tunajisogeza kwao kutokana
na fedha walizo nazo. Inatakiwa tujifunze ufahamu walio nao kuhusu fedha. Na
kuna pointi moja hapa naomba kuiongeza,watu wenye fedha maongezi yao huwa ya
fedha na wala sikutanii ni kweli kabisa. Wao hufurahishwa na fedha wanatamani
kuziongeza na sio kuzipunguza.kwa hiyo ukiwa na marafiki wenye fedha utajifunza
kutoka kwao jinsi ya kupata fedha, kuziongeza na kuzitunza.
Na angalia marafiki ambao
hawana fedha hawapendi kuongea kuhusu fedha, biashara wala uwekezaji. Na
ukianza kuongea masuala ya fedha wakiwapo wanaona kama vile unaleta mikogo.
Usiwaepe hao pia kwani kutoka kwao utajifunza usifanye nini kitakachokurudisha
au kukuingiza katika ufukara. Hebu waulize marafiki zako wenye hela kama wana
marafiki mafukara ambao wanafika kuuliza walifanya vipi kuukwaa utajiri, zaidi
zaidi watakueleza mara nyingi marafiki wa namna hiyo wajapo kwao huja kwa nia
hizi kama si zaidi ya hizi
1. kuomba msaada
2. kukopa
3. kuomba kazi.
Ni vema kutofuata ushauri
wa watu masikini watu waliochanganyikiwa na maisha. Tusiwatenge ,tuwapende kwa
dhati lakini inapofika masuala ya fedha au uwekezaji watakuambia biashara hii
haitakulipa kuna watu wanawasikiliza na mambo yanawaendea kombo tatizo ni
kwamba walisikiliza ushauri na kuufuata bila kudadisi kiundani na hawana sababu
ya kulaumu wanapoanguka kwani wamesahau kuwa
“ndege wa mbawa moja huruka pamoja”. Unatakiwa kuwa makini sikiliza watu
wote, fungua akili yako kwasababu unakuwa na mawazo yanayotofautiana na baada
ya hapo utagundua yapi ni mawazo ya mtu tajiri na yapi ni ya mtu masikini.
Hakika jambo moja gumu
kuwa tajiri ni kuwa mkweli kwa nafsi yako,na kujiepusha kufuata mkumbo yaani
kufuata kile anachofanya kila mtu. Hebu fikiri juu ya dili linalotangazwa
katika ukurasa wa mbele katika gazeti wao huita (front page) usilifuatilie
umechelewa tafuta dili jingine, mlango mmoja unapofungwa mwingine unafunguliwa.
Ukifuatana na marafiki matajiri utazijua dili kabla hazijafika “front page” kwa wafuata mkumbo, utajua
mambo ya ndani kabla hayajafika nje na unapokuwa tayari umetengeneza faida ndio
wengine wanaingia wakati wewe unatoka.
4: nini au nani anakuvutia.?
Kwa njia Fulani kuna mambo
yanawezekana. Hivi ulipokuwa mdogo ni mtu gani ulipenda kuwa kama yeye (your
child hero). Nilipokuwa mdogo nilipenda sana kuwa mwandishi wa vitabu kama
Chinua Achebe, Ngugi Wa Thiong’o na James Hadley Chase. Kama watu niliojivunia
nilijitahidi sana kusoma vitabu vyao kwa mfano nilijikuta nimesoma vitabu kama
25 vya Chase na nilivinunua kwa gharama yoyote ile hata ikibidi kutumia fedha
yangu ya chakula shuleni. Nilihitaji kujua maisha ya watu hao, wametokea wapi
mpaka kufika hapo walipo, kipato chao. Nilihitaji kujua kila kitu kuhusu wao
kwasababu nilitaka kuwa kama wao.
Kutokana na hali hiyo
nilitokea kuiongea lugha ya kingereza kwa ufasaha na kuchaguliwa kuwa
mwenyekiti wa debate club shuleni. Wakati huo sikuwa mimi nilikuwa Chase, Ngugi
na Chinua, lakini je hatimaye nilikuwa wao loh!! Niliwapoteza mashujaa wangu,
heroes wangu kadili nilivyoendelea kuwa mtu mzima.
Leo hii waulize watoto
wanataka kuwa kama nani… hapo utasikia nataka kuwa kama Obama, Michael Jordan, Bill Gate, Lily Wayne,mwalimu Nyerere,Lady Jay D ( Judith Wambula), Erick Shigongo nk.Hawana kosa wanastahili kufanya
hivyo kwani hiyo inawafanya kuwa na mtizamo kama watu hao maadamu tu wanaiga
watu wale ambao wana mchango katika jamii unaotambulika na wa mfano bora wa
kuigwa. Na ndio maana watu hao wakifanya jambo linaloikera jamii watu hupiga
kelele sana kwani kufanya kwao maovu huwapotosha vijana wanaotamani kuwa kama
wao.
Unafikiri itakuwa vema kwa
mtu kama Erick Shigongo kuwa fisadi,hatutajisikia vibaya kwa yeye kupelekwa
mahakamani tu bali atapoteza mashujaa wengi,vijana wanaojitahidi kuishi na kuwa
kama yeye ghafra wanatakiwa kumsahau shujaa wao je unaufahamu msemo usemao “mti
mkubwa unapoanguka huangukia miti midogo inayojitahidi kukua chini ya kimvuli
chake” Sio kwamba kuwa hero kunakufanya uwavutie watu au kuwafurahisha tu
hapana bali unafanya maisha kwao yawe rahisi kwani wakati wote watu watasema
kama Reginard Mengi ameweza kwanini mimi nishindwe????. Inapofikia suala la
kuanza biashara na kuwekeza watu wengi huona kama ni jambo gumu hilo lakini
wanaona inakuwa rahisi wanapowafikilia mashujaa wao.
5: tunapata kuliko tunavyotoa
Kuna nguvu Fulani
iliyofichika kuhusu kutoa. Kuna kitu unapaswa kukifanya katika maisha yako yote
ni kujitolea pale inapobidi. Wape watu fedha, muda, pamoja na ufahamu pale
inapobidi. Kama unataka kitu basi toa kitu kwanza. Ukijikuta una uhitaji wa
fedha hebu saidia vikundi vinavyotoa huduma kwa jamii bila faida. Toa kwanza
kile unachohitaji na ndipo utapata kwa
mamilioni sio wewe unahitaji tu na wala hutoi. Watu wengi najua hawataweza
kufanya hivyo lakini amini usiamini ni jambo ambalo hakika huwa lina jibu, tena
jibu chanya sio hasi.
Kama unaona hilo ni gumu
basi wewe bado una fikra za kimasikini, bado unawaza kama mtu masikini kwani
watu masikini daima ni wabinafsi sana kuliko watu tajiri. Kama mtu ni tajiri
basi ujue anafanya kitu katika jamii ambacho watu wanakihitaji. Hivi ni busara
kweli kwenda TANESCO na kuwaambia mkinipa umeme nitawapa fedha sijui kama kweli
utapata kama usipotoa fedha.
Ni kweli kwamba unaweza
kufanikiwa ukiwa peke yako lakini utafanikiwa haraka na zaidi kama ukiwa na
wengine.
Tutaendelea na sehemu ya 3


