Tuesday, 18 November 2014

NAMNA YA KUANZA SAFARI YA UTAJIRI - SEHEMU YA 2

2: chagua

Katika kila shilingi unayopata na kuishika mkononi una uhuru wa kuchagua mstakabali wako wa kuwa tajiri au masikini au mtu wa daraja la kati. Namna yako ya matumizi inaeleza wazi wazi wewe ni mtu wa namana gani. Kwa hiyo katika wakati huu ulio nao chagua kuwa tajiri. Na ukitaka kuwa tajiri jifunze namana ya kumiliki mali, mali ya kweli na sio ya kupita. Vijana wengi hurithi mali kutoka kwa wazazi wao na huipoteza bila kujua kwasababu hawajifunzi namna ya kuitunza, hivyo hata tukirithi mali bado tuna jukumu la kujifunza namna ya kuitunza na kuifanya iwe mali ya kweli.
Watu wengi huchagua kubaki masikini kutokana na kuwa na imani mbalimbali wengine husema “mimi sipendi hela”, “hamna shida mimi bado kijana bado nina muda”, “nikipata hela ya kutosha ndio nitafikiria nini cha kufanya”, “hamna shida mbona baba yangu ana fedha ya kutosha”. Mawazo kama hayo yanamfanya mtu afikie upeo wake wa kufikiri. Hata kama huna fedha jifunze juu ya kuzimiliki. Lakini bado tunabaki na uamuzi wa kuchagua kila siku; nini cha kufanya na muda wetu,fedha zetu,na nini cha kuwaza katika vichwa vyetu chaguo liko juu yetu. Na huo ndio uhuru wa kuchagua uhuru ambao kila mtu anao na ana wajibu wa kuutumia, uhuru wa kuchagua kuwa tajiri na tuna takiwa kuchagua kuwa matajiri kila siku ya maisha yetu.


WEKEZA KATIKA ELIMU;

Hakuna mtu anayeweza kukunyang’anya akili. Akili ndio mali pekee ambayo binadamu amejaliwa. Kila mtu ana uhuru wa kuchagua nini cha kuweka katika ubongo wake mala tu anapokuwa mtu mzima. Nyingi kati ya biashara zetu hufa kwasababu tunazianzisha kabla ya kujifunza namna ya kuendesha biashara. Hata leo hii naaandika kitabu kinachogusa maisha yetu ya kila siku lakini sijui ni watu wangapi watakihitaji na kukinunua badala ya kutumia fedha zao kununua pombe na CD za muziki na filamu. Wengi wetu tumeishia kununua TV na VCR,VCD, DVD n.k na ni wachache sana wanaonunua vitabu. Huo ndio uhuru wa kuchagua, ambao unabaki mikononi mwa kila mtu binafsi.

3: marafiki
Ushirikiano ndio nguzo ya mafanikio, utafanya ushirikiano na nani?. Hakika jibu litakuwa ni marafiki, ONYO, chagua marafiki na wala usiwachague kutokana na uwezo walio nao kiuchumi. Tuwe na marafiki, wawe mamilionea au mafukara nia hasa ni kujifunza kutoka kwao wote tena kwa ufahamu wa hali ya juu.
Namna yetu ya kujumuika na marafiki tajiri iwe ya makini wasije wakahisi kuwa tunajisogeza kwao kutokana na fedha walizo nazo. Inatakiwa tujifunze ufahamu walio nao kuhusu fedha. Na kuna pointi moja hapa naomba kuiongeza,watu wenye fedha maongezi yao huwa ya fedha na wala sikutanii ni kweli kabisa. Wao hufurahishwa na fedha wanatamani kuziongeza na sio kuzipunguza.kwa hiyo ukiwa na marafiki wenye fedha utajifunza kutoka kwao jinsi ya kupata fedha, kuziongeza na kuzitunza.
Na angalia marafiki ambao hawana fedha hawapendi kuongea kuhusu fedha, biashara wala uwekezaji. Na ukianza kuongea masuala ya fedha wakiwapo wanaona kama vile unaleta mikogo. Usiwaepe hao pia kwani kutoka kwao utajifunza usifanye nini kitakachokurudisha au kukuingiza katika ufukara. Hebu waulize marafiki zako wenye hela kama wana marafiki mafukara ambao wanafika kuuliza walifanya vipi kuukwaa utajiri, zaidi zaidi watakueleza mara nyingi marafiki wa namna hiyo wajapo kwao huja kwa nia hizi kama si zaidi ya hizi
 1. kuomba msaada
 2. kukopa 
 3. kuomba kazi.
Ni vema kutofuata ushauri wa watu masikini watu waliochanganyikiwa na maisha. Tusiwatenge ,tuwapende kwa dhati lakini inapofika masuala ya fedha au uwekezaji watakuambia biashara hii haitakulipa kuna watu wanawasikiliza na mambo yanawaendea kombo tatizo ni kwamba walisikiliza ushauri na kuufuata bila kudadisi kiundani na hawana sababu ya kulaumu wanapoanguka kwani wamesahau kuwa  “ndege wa mbawa moja huruka pamoja”. Unatakiwa kuwa makini sikiliza watu wote, fungua akili yako kwasababu unakuwa na mawazo yanayotofautiana na baada ya hapo utagundua yapi ni mawazo ya mtu tajiri na yapi ni ya mtu masikini.
Hakika jambo moja gumu kuwa tajiri ni kuwa mkweli kwa nafsi yako,na kujiepusha kufuata mkumbo yaani kufuata kile anachofanya kila mtu. Hebu fikiri juu ya dili linalotangazwa katika ukurasa wa mbele katika gazeti wao huita (front page) usilifuatilie umechelewa tafuta dili jingine, mlango mmoja unapofungwa mwingine unafunguliwa. Ukifuatana na marafiki matajiri utazijua dili kabla hazijafika “front page” kwa wafuata mkumbo, utajua mambo ya ndani kabla hayajafika nje na unapokuwa tayari umetengeneza faida ndio wengine wanaingia wakati wewe unatoka.

4: nini au nani anakuvutia.?

Kwa njia Fulani kuna mambo yanawezekana. Hivi ulipokuwa mdogo ni mtu gani ulipenda kuwa kama yeye (your child hero). Nilipokuwa mdogo nilipenda sana kuwa mwandishi wa vitabu kama Chinua Achebe, Ngugi Wa Thiong’o na James Hadley Chase. Kama watu niliojivunia nilijitahidi sana kusoma vitabu vyao kwa mfano nilijikuta nimesoma vitabu kama 25 vya Chase na nilivinunua kwa gharama yoyote ile hata ikibidi kutumia fedha yangu ya chakula shuleni. Nilihitaji kujua maisha ya watu hao, wametokea wapi mpaka kufika hapo walipo, kipato chao. Nilihitaji kujua kila kitu kuhusu wao kwasababu nilitaka kuwa kama wao.
Kutokana na hali hiyo nilitokea kuiongea lugha ya kingereza kwa ufasaha na kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa debate club shuleni. Wakati huo sikuwa mimi nilikuwa Chase, Ngugi na Chinua, lakini je hatimaye nilikuwa wao loh!! Niliwapoteza mashujaa wangu, heroes wangu kadili nilivyoendelea kuwa mtu mzima.
Leo hii waulize watoto wanataka kuwa kama nani… hapo  utasikia nataka kuwa kama Obama, Michael Jordan, Bill Gate, Lily Wayne,mwalimu Nyerere,Lady Jay D ( Judith Wambula), Erick Shigongo nk.Hawana kosa wanastahili kufanya hivyo kwani hiyo inawafanya kuwa na mtizamo kama watu hao maadamu tu wanaiga watu wale ambao wana mchango katika jamii unaotambulika na wa mfano bora wa kuigwa. Na ndio maana watu hao wakifanya jambo linaloikera jamii watu hupiga kelele sana kwani kufanya kwao maovu huwapotosha vijana wanaotamani kuwa kama wao.
Unafikiri itakuwa vema kwa mtu kama Erick Shigongo kuwa fisadi,hatutajisikia vibaya kwa yeye kupelekwa mahakamani tu bali atapoteza mashujaa wengi,vijana wanaojitahidi kuishi na kuwa kama yeye ghafra wanatakiwa kumsahau shujaa wao je unaufahamu msemo usemao “mti mkubwa unapoanguka huangukia miti midogo inayojitahidi kukua chini ya kimvuli chake” Sio kwamba kuwa hero kunakufanya uwavutie watu au kuwafurahisha tu hapana bali unafanya maisha kwao yawe rahisi kwani wakati wote watu watasema kama Reginard Mengi ameweza kwanini mimi nishindwe????. Inapofikia suala la kuanza biashara na kuwekeza watu wengi huona kama ni jambo gumu hilo lakini wanaona inakuwa rahisi wanapowafikilia mashujaa wao.


5: tunapata kuliko tunavyotoa
Kuna nguvu Fulani iliyofichika kuhusu kutoa. Kuna kitu unapaswa kukifanya katika maisha yako yote ni kujitolea pale inapobidi. Wape watu fedha, muda, pamoja na ufahamu pale inapobidi. Kama unataka kitu basi toa kitu kwanza. Ukijikuta una uhitaji wa fedha hebu saidia vikundi vinavyotoa huduma kwa jamii bila faida. Toa kwanza kile unachohitaji  na ndipo utapata kwa mamilioni sio wewe unahitaji tu na wala hutoi. Watu wengi najua hawataweza kufanya hivyo lakini amini usiamini ni jambo ambalo hakika huwa lina jibu, tena jibu chanya sio hasi.
Kama unaona hilo ni gumu basi wewe bado una fikra za kimasikini, bado unawaza kama mtu masikini kwani watu masikini daima ni wabinafsi sana kuliko watu tajiri. Kama mtu ni tajiri basi ujue anafanya kitu katika jamii ambacho watu wanakihitaji. Hivi ni busara kweli kwenda TANESCO na kuwaambia mkinipa umeme nitawapa fedha sijui kama kweli utapata kama usipotoa fedha.
Ni kweli kwamba unaweza kufanikiwa ukiwa peke yako lakini utafanikiwa haraka na zaidi kama ukiwa na wengine.

Tutaendelea na sehemu ya 3















so its our duty to make people understand






Monday, 17 November 2014

NAMNA YA KUANZA SAFARI YA UTAJIRI

     "Successful people are simply those with successful habits.”

     Natamani kusema kuwa kupata utajiri ni kitu rahisi, lakini nashindwa kwani sio hivyo. Na kama sio rahisi swali bado linabaki nitaanza vipi kuusaka utajiri?. Kwa wachimbaji wa dhahabu wanajua kwamba kuna dhahabu katika eneo lote la machimbo, lakini hawana utaalamu wa jinsi ya kuziona. Kwa hakika ni rahisi kupata dili za maana sana katika dunia hii. Lakini inapofikia suala la pesa inahitaji makusudio ya dhati kabisa kwa mtu anayezihitaji.
         Kupata dili litakalokutoa kimaisha inahitajika kuwa na ufahamu wa fedha. Naamini kuwa kila mtu ana ufahamu kuhusu fedha, lakini tatizo ni kwamba bado tumelala usingizi na tunahitaji kuamshwa. Kwa hakika tumelala usingizi kwa kutegemea kupata utajiri kutokana na ushirikina.
        Kuna ile dhana nyigine eti “ kupenda fedha ndio chanzo cha maovu yote “. Dhana hiyo imetufanya tuanguke katika mtego wa kusoma na kufanya kazi kwa ajili ya kupata pesa, tumeshindwa kuuona ukweli kwamba fedha zinaweza kufanya kazi kwa ajili yetu. Tumesahau kuwa na hofu juu ya hali yetu ya kifedha ya kesho, tunasubili kuja kuwatesa watu wengine kwa kuwa tegemezi pale tutakapokuwa hatuwezi kufanya kazi tena.
         Hakika maisha hayo ni ya hatari sana, kwani tutawapa taabu sana watoto wetu ambao tumewarithisha mfumo uleule wa umasikini. Inatakiwa tubadilike, tusijirahisishe kwa kukimbilia kuajiliwa. Kwa hakika maisha tunayoishi ni ya kufuata mkumbo ati kwasababu Fulani kafanya hivi basi na wewe unataka kufanya vivyo hivyo.
       Kuna dhahabu kila mahali lakini watu hawajafundishwa namna ya kuziona. Mtu wa kawaida atakwenda kila mahali mgodini lakini hawezi kuziona dhahabu. Je wewe unataka kuziona dhahabu?
Basi fuatana nami ili tujue jinsi ya kutumia na kuendeleza vipaji alivyotupa mungu badala ya kutegemea hilizi na kuuwa binadamu wenzetu kwa minajili ya kupata utajili.

1: Je Una sababu?

      Una nia ile kutoka moyoni? Watu wengi sana wanapenda kuwa matajiri na kujikwamua kiuchumi, lakini hawana nia ile ya kweli. Barabara ya kuuelekea utajiri kwao imekuwa ni ndefu mno na milima ya kupanda ni mingi mno, hivyo kujikuta wakikata tamaa na kuona ni bora kurejea katika hali ya awali.
     Kuwa na sababu, dhumuni na uhitaji na sio kusema sihitaji na hata ukiulizwa kwa nini unataka kuwa tajiri ni lazima uwe na sababu. Je unahitaji kufanya kazi maisha yako yote, je unahitaji kuajiliwa na kulazimishwa kufanya hata yale usiyotaka, unataka kufa na kuacha familia yako masikini. Najua wengi majibu yetu ni sio, lakini je tuna ile nia ya kutoka moyoni ya kusema hapana kwa maswali hayo hapo juu.
    Nadhani hatimaye tukifanya kazi kwa uaminifu na kupata kipato cha kutufanya tuwe matajiri tuna weza, kuzunguka katika dunia hii na kuishi maisha tunayoyataka, tutakuwa huru kumiliki muda na maisha yetu na hatimaye hatutakuwa watumwa wa pesa bali pesa ndio itakuwa mtumwa wetu.
     Siwezi kuacha kusema tena “unatakiwa uwe na sababu na nia kwa nini unataka kuwa tajiri??” Haya safari kuelekea utajiri ni ndefu sana na waweza kurudi nyuma sana wakati mwingine, lakini kama una ile nia ya kweli utasimama tena na kusonga mbele. Waingereza wana msemo wao “life starts at 40”. Huu ni ujumbe kwa vijana kabla ya kufikisha miaka 40 unatakiwa uwe umetengeneza maisha yako uwe huru kiuchumi.
Je kupata utajiri ni rahisi?. Sio rahisi na wala sio vigumu pia lakini ukweli ni kwamba bila kuwa na sababu, nia na dhumuni kila kitu ni kigumu katika maisha.

TUMAINI KWA WAKULIMA WA KAKAO (COCOA)

 Kakao ni zao linalotumika kutengeneza vitu vitamu sana kama chocolate na ice cream. Ni zao ambalo kwa Tanzania linastawi sana katika mikoa ya Mbeya wilayani Kyela, Busokelo na Ileje na katika mkoa wa Morogoro.
Wiki nzima tumekuwa tukitengeneza documentary ambayo itatumika katika matangazo ya kutangaza bidhaa zitokanazo na kakao. Matangazo hayo yanatengenezwa na UNILIVER  kupitia kitengo chao cha utengenezaji wa chocolate cha MAGNUM.
Matangazo hayo yataonyeshwa katika nchi za ulaya hasa zenye walaji wa bidhaa za chocolate. Shukrani za zati ziende kwa kampuni ya BIOLANDS Kyela kwa kufanikisha ujio huo.
Ni matumaini yetu kwamba baada ya matangazo hayo kuanza kurushwa huko ulaya itaongeza walaji wa bidhaa za kakao na hivyo kufanya zao hilo kuwa na bei nzuri kwa wakulima nahatimae waweze kupata premium kwa mazao yao.
Hata mimi mwana blog mwenzako nilipata nafasi ya kukutana na wageni kutoka nchi za ulaya kama vile Sweden na Uingereza, na kizuri zaidi nimealikwa niende kutembelea nchi zote walikotoka hao na kwamba watakuwa wenyeji wangu,,,wana blog je nauri hizo nitatoa wapi??.
Hapa chini nawapa vionjo muweze kuona baadhi ya picha tulizopiga nitaendelea kuwatupia kidogo kidogo siku hadi siku.
Na pia ni fursa sasa kwa wakulima wa kakao kuongeza uzalishaji wa kakao na iliyo bora, kwa kuwa sasa hivi kutokana na ushindani wa kibiashara watu wameacha kabisa kufuata kanuni bora za kilimo. Jamani tuachane na ujinga huo hebu tuelimike na tujue kuwa kakao ni chakula na hivyo tufuate kanuni bora za kilimo tuache kuwatumia wafanyabiashara waitwao njemke hao kwa hakika baada ya muda watkuja kuharibu zao la kakao.

HEBU TIZAMA PICHA HIZI HAPA CHINI.
Ni asubuhi katika milima ya Livingstone tukianza maandalizi ya shooting.





Mti wa kakao ukiwa na matunda.



Shooting inaendelea katika ofisi za BIOLANDS Kyela ikionyesha kakao inavyochambuliwa.


Kakao ikiwa imeanikwa katika ofisi za BIOLANDS Kyela ili kufikia unyevu unaotakiwa.



Wadau wa zao la kakao hao Bw. Ephraem Mwandambo ( katikati ), Expeditor Nzalalila ( kushoto ) na Frank Samwel ( kulia )  wakiwa katika shamba darasa  la kakao. Hawa jamaa ni shiiida katika zao la kakao yaani wamebobea.



ikianikwa juu ya vichanja katika usafi wa hali ya juu ili kuhakikisha ubora unadhibitiwa



Friday, 14 November 2014

INSPIRATION QUOTES


kwa wenzangu wanaojua umombo tutakuwa nazo hizi kila wakati na kwa wengine tupieni hapa hata za kiswahili nitathamini sana mchango wa kila mtu.


  • 1.       Do you wish to rise? Begin by descending." 
  • "Do nothing from selfishness or empty conceit, but with humility of mind, let each regard one another as more important than himself; do not merely look out for your own personal interests, but also for the interests of others."
  • A good leader is a good listener..
  • 2.       “Landlords grow rich in their sleep.” 
  • 3.       To be successful, the first thing to do is fall in love with your work
  • 4.       People often fear that if they're real, nobody will like them, but the key to success is genuineness.
  • 5.       When we invest in women, we invest in those who invest in everybody else. Data has helped us understand that women and men spend money differently, and women are more likely invest in their children.
  • 6.       "Some people plant in the spring and leave in the summer. If you’ve signed up for a season, see it through. You don’t have to stay forever, but at least stay until you see it through." -- Jim Rohn
  • 7.       Remembering that you are going to die is the best way I know to avoid the trap of thinking you have something to lose. You are already naked, there is no reason not to follow your heart - Steve Jobs
  • 8.       For we cannot completely understand where we are unless we first understand where we’ve been.
  • 9.       Those who fail to plan, plan to fail.” 
  • 10.    Thinking is the hardest work there is, which is probably the reason why so few engage in it!!
  • 11.    To get from where you're at to where you want to be, you have to step out in faith. Take the leap and your wings will appear.

HEBU TUCHEKE KIDOGO KWA LEO

haya mr. waziri
Waziri wa ufugaji katembelea mradi wa NYUKI, alipofika getini Mlinzi akamwambia haruhusiwi mtu kuingia kwa sasa!
Waziri kwa hasira akamjibu Mlinzi kwani hujui mimi ni nani huku akimwonesha kitambulisho!
Mlinzi kwa utii, akamwambia haya ingia muheshimiwa!
Baada ya muda mfupi, Waziri alisikika akiita Mlinzi, Mlinzi NYUKI wamenivamia-Mlinzi AKAJIBU waoneshe kitambulisho huenda HAWAKUJUI WEWE NI NANI


NYINGINE ( unajua umombo wewe hebu check hii ) 

A guy went for an interview at a big IT company for the position of 'Computer Hacking Investigator.'
The boss asked him, "So, what makes you suitable for this job?"
"Well," he replied, "I hacked into your computer and invited myself to this interview."
1.    
                               haya nisije maliza yote tutaonana tena na kucheka siku nyingine

Friday, 7 November 2014

BAJETI



Wewe ni sawa na kila mtu kama ukifikiri hivyo, lakini ukifikiri tofauti basi ndivyo ulivyo. 


Kila inapofika katikati ya mwezi watu wengi hujiuliza nini wamefanya kutokana na mshahara wao. Wengine huhisi kama vile hawakupata kipato chochote, kwa vile huwa hawana kilichobaki. Hayo yote hutukuta kwasababu hatuna utaratibu katika matumizi ya fedha zetu.
Kuwa huru kiuchumi haitegemei kiasi gani cha fedha unapata kila mwezi au mwaka, bali ni namna unavyotumia fedha hizo katika njia inayofaa. Namna pekee ya kukuwezesha kutumia fedha zako kwa utaratibu ni kutengeneza bajeti yako;utaratibu wa matumizi yako ya fedha.
Kutengeneza bajeti yako binafsi sio kitu kigumu sana na wala haikuhitaji kuwa na digrii, wala hauhitaji kuwa na sifa za ajabu. Kwa kweli bajeti ni mlolongo wa mapato na matumizi na wala sio kitu kingine.

Unahitaji kujua Kipato chako

Kabla ya kuanza kuandaa bajeti yako unahitaji kujua kipato chako kwa sasa. Chukua karatasi na andika mapato yako yote ambayo una uhakika nayo kila mwezi na zidisha mara 12, tarakimu unayoipata ndio kipato chako cha mwaka na hicho ndio kiasi kitakachukuwezesha kuishi kwa mwaka mzima.
kwa hiyo ni jukumu lako sasa kujikwamua kiuchumi kwa kupangilia jinsi gani utatumia kipato chako hicho.

Vipi kuhusu matumizi yako

Hebu chukua karatasi 12 tena na andika jina la kila mwezi katika karatasi hizo. Chukua karatasi ya januari na andika matumizi yote unayotegemea kutumia katika mwezi huo. Nafikiri hilo pia halitakuwa gumu kwani kila mtu anajua kiasi gani anatumia kila mwezi na kwa vitu gani.
Kwa hakika matumizi yetu yamegawanyika katika sehemu zifuatazo

  1. Matumizi ya lazima ambayo hayabadiliki mara kwa mara.
kodi ya nyumba,
mkopo,
bima,
ada ya shule,
ada za usajiri nk.

  1. Matumizi ya lazima ambayo hubadilika.
Nauri,
Umeme,
Simu,
Chakula,
Matibabu,
Akiba,nk.

  1. Matumizi yasiyo ya lazima.

Nguo,
Magazeti,
Zawadi za sikukuu,
Pombe,
Sigara,nk

Jumlisha matumizi ya sehemu zote hizo tatu hapo juu kwa kila mwezi, na hiyo ndio gharama ya wewe kuishi kwa mwaka.

Je unaishi au unasindikiza wengine

Unaweza kujua kama unaishi endapo kipato chako kinazidi gharama ya matumizi yako kwa mwaka.

Lakini pia unaweza kufanya mabadiliko

Angalia hizo sehemu tatu za matumizi hapo juu. Namna pekee ya kukufanya uishi ni kwa kuwa na kipato kikubwa na matumizi kidogo, kwa hiyo njia pekee ni kupunguza matumizi ili kuwa na fedha za ziada.
Sehemu pekee ambapo tunaweza kufanya mabadiliko ni namba 2 na 3 kwani kufanya mabadiliko katika namba 1 huweza pia kuathiri maisha yetu. Matumizi ya lazima ambayo hubadilika na matumizi yasiyo ya lazima huwaingiza watu katika matatizo makubwa sana kufanya maamuzi na ni katika sehemu hii ambapo watu wangeweza kujipatia kipato cha ziada.
Bila kupangilia matumizi ya fedha watu wengi hujikita katika kununua hata vitu wasivyovihitaji, na hivyo kujikuta hawana akiba. Wataalamu wengi wa mambo ya uchumi wanashauri mtu atunze 10% ya kipato chake, hivyo upatapo kipato tenga fedha kwaajili ya matumizi ya lazima yasiyobadilika na weka akiba ndipo uanze matumizi kwa vitu vinavyobadilika na kwa vile visivyo vya lazima kwani hata tukivikosa bado tunaweza kuishi. Kama usipofanya hivyo utaendelea kuishi kwa shida na maumivu.

Namana ya kupunguza matumizi

·         Tumia kile ulicho nacho tu kwa makini.
·         Usitumie chote upatacho leo ili uweze kutumia na kesho hadi kifo chako.
·         Punguza matumizi kwa vitu kama sigara,vinywaji, mikate, keki, chokoleti, simu nk.
·         Matumizi ya gali kama unalo.
·         Nguo.
·         Matamasha na starehe

Sio nia yangu kuwazuia watu wasifanye starehe hata kidogo; hapana nia ni kuwafanya watu wawe na nidhamu katika matumizi yao ya fedha na huko ndio kuweka maisha yako katika msimamo kwa kufanya maamuzi ya busara. Unahitajika kujijengea nidhamu ya hali ya juu na kuhitajika kufanya maamuzi ambayo wakati mwingine yatakuwa ni magumu, namna pekee ya kubadilisha maisha yako ni kwa wewe kubadilika na hata kama kipato chako ni kidogo hamna shida utafika tu maadamu ukibadilika. Namna pekee ya kufanikiwa kiuchumi ni kupunguza matumizi ili kuwa na kipato cha ziada la bila hivyo utakuwa unashika kisu katika makali na ukiwaza ni lini mpini wa kisu utavutwa.