BAJETI
Wewe ni sawa na kila mtu kama ukifikiri hivyo, lakini ukifikiri tofauti basi ndivyo ulivyo.
Kila inapofika katikati ya
mwezi watu wengi hujiuliza nini wamefanya kutokana na mshahara wao. Wengine
huhisi kama vile hawakupata kipato chochote, kwa vile huwa hawana kilichobaki.
Hayo yote hutukuta kwasababu hatuna utaratibu katika matumizi ya fedha zetu.
Kuwa huru kiuchumi
haitegemei kiasi gani cha fedha unapata kila mwezi au mwaka, bali ni namna
unavyotumia fedha hizo katika njia inayofaa. Namna pekee ya kukuwezesha kutumia
fedha zako kwa utaratibu ni kutengeneza bajeti yako;utaratibu wa matumizi yako
ya fedha.
Kutengeneza bajeti yako
binafsi sio kitu kigumu sana na wala haikuhitaji kuwa na digrii, wala hauhitaji
kuwa na sifa za ajabu. Kwa kweli bajeti ni mlolongo wa mapato na matumizi na
wala sio kitu kingine.
Unahitaji kujua Kipato chako
Kabla ya
kuanza kuandaa bajeti yako unahitaji kujua kipato chako kwa sasa. Chukua karatasi
na andika mapato yako yote ambayo una uhakika nayo kila mwezi na zidisha mara
12, tarakimu unayoipata ndio kipato chako cha mwaka na hicho ndio kiasi
kitakachukuwezesha kuishi kwa mwaka mzima.
kwa hiyo ni
jukumu lako sasa kujikwamua kiuchumi kwa kupangilia jinsi gani utatumia kipato
chako hicho.
Vipi kuhusu matumizi yako
Hebu chukua
karatasi 12 tena na andika jina la kila mwezi katika karatasi hizo. Chukua
karatasi ya januari na andika matumizi yote unayotegemea kutumia katika mwezi
huo. Nafikiri hilo pia halitakuwa gumu kwani kila mtu anajua kiasi gani
anatumia kila mwezi na kwa vitu gani.
Kwa hakika
matumizi yetu yamegawanyika katika sehemu zifuatazo
- Matumizi
ya lazima ambayo hayabadiliki mara kwa mara.
kodi ya
nyumba,
mkopo,
bima,
ada ya
shule,
ada za
usajiri nk.
- Matumizi
ya lazima ambayo hubadilika.
Nauri,
Umeme,
Simu,
Chakula,
Matibabu,
Akiba,nk.
- Matumizi
yasiyo ya lazima.
Nguo,
Magazeti,
Zawadi za
sikukuu,
Pombe,
Sigara,nk
Jumlisha
matumizi ya sehemu zote hizo tatu hapo juu kwa kila mwezi, na hiyo ndio gharama
ya wewe kuishi kwa mwaka.
Je unaishi au unasindikiza wengine
Unaweza
kujua kama unaishi endapo kipato chako kinazidi gharama ya matumizi yako kwa
mwaka.
Lakini pia unaweza kufanya mabadiliko
Angalia hizo
sehemu tatu za matumizi hapo juu. Namna pekee ya kukufanya uishi ni kwa kuwa na
kipato kikubwa na matumizi kidogo, kwa hiyo njia pekee ni kupunguza matumizi
ili kuwa na fedha za ziada.
Sehemu pekee
ambapo tunaweza kufanya mabadiliko ni namba 2 na 3 kwani kufanya mabadiliko
katika namba 1 huweza pia kuathiri maisha yetu. Matumizi ya lazima ambayo
hubadilika na matumizi yasiyo ya lazima huwaingiza watu katika matatizo makubwa
sana kufanya maamuzi na ni katika sehemu hii ambapo watu wangeweza kujipatia
kipato cha ziada.
Bila
kupangilia matumizi ya fedha watu wengi hujikita katika kununua hata vitu
wasivyovihitaji, na hivyo kujikuta hawana akiba. Wataalamu wengi wa mambo ya
uchumi wanashauri mtu atunze 10% ya kipato chake, hivyo upatapo kipato tenga
fedha kwaajili ya matumizi ya lazima yasiyobadilika na weka akiba ndipo uanze
matumizi kwa vitu vinavyobadilika na kwa vile visivyo vya lazima kwani hata
tukivikosa bado tunaweza kuishi. Kama usipofanya hivyo utaendelea kuishi kwa
shida na maumivu.
Namana ya kupunguza matumizi
·
Tumia kile ulicho nacho tu kwa
makini.
·
Usitumie chote upatacho leo ili uweze
kutumia na kesho hadi kifo chako.
·
Punguza matumizi kwa vitu kama
sigara,vinywaji, mikate, keki, chokoleti, simu nk.
·
Matumizi ya gali kama unalo.
·
Nguo.
·
Matamasha na starehe
Sio nia
yangu kuwazuia watu wasifanye starehe hata kidogo; hapana nia ni kuwafanya watu
wawe na nidhamu katika matumizi yao ya fedha na huko ndio kuweka maisha yako
katika msimamo kwa kufanya maamuzi ya busara. Unahitajika kujijengea nidhamu ya
hali ya juu na kuhitajika kufanya maamuzi ambayo wakati mwingine yatakuwa ni
magumu, namna pekee ya kubadilisha maisha yako ni kwa wewe kubadilika na hata
kama kipato chako ni kidogo hamna shida utafika tu maadamu ukibadilika. Namna
pekee ya kufanikiwa kiuchumi ni kupunguza matumizi ili kuwa na kipato cha ziada
la bila hivyo utakuwa unashika kisu katika makali na ukiwaza ni lini mpini wa
kisu utavutwa.
No comments:
Post a Comment