Monday, 17 November 2014

NAMNA YA KUANZA SAFARI YA UTAJIRI

     "Successful people are simply those with successful habits.”

     Natamani kusema kuwa kupata utajiri ni kitu rahisi, lakini nashindwa kwani sio hivyo. Na kama sio rahisi swali bado linabaki nitaanza vipi kuusaka utajiri?. Kwa wachimbaji wa dhahabu wanajua kwamba kuna dhahabu katika eneo lote la machimbo, lakini hawana utaalamu wa jinsi ya kuziona. Kwa hakika ni rahisi kupata dili za maana sana katika dunia hii. Lakini inapofikia suala la pesa inahitaji makusudio ya dhati kabisa kwa mtu anayezihitaji.
         Kupata dili litakalokutoa kimaisha inahitajika kuwa na ufahamu wa fedha. Naamini kuwa kila mtu ana ufahamu kuhusu fedha, lakini tatizo ni kwamba bado tumelala usingizi na tunahitaji kuamshwa. Kwa hakika tumelala usingizi kwa kutegemea kupata utajiri kutokana na ushirikina.
        Kuna ile dhana nyigine eti “ kupenda fedha ndio chanzo cha maovu yote “. Dhana hiyo imetufanya tuanguke katika mtego wa kusoma na kufanya kazi kwa ajili ya kupata pesa, tumeshindwa kuuona ukweli kwamba fedha zinaweza kufanya kazi kwa ajili yetu. Tumesahau kuwa na hofu juu ya hali yetu ya kifedha ya kesho, tunasubili kuja kuwatesa watu wengine kwa kuwa tegemezi pale tutakapokuwa hatuwezi kufanya kazi tena.
         Hakika maisha hayo ni ya hatari sana, kwani tutawapa taabu sana watoto wetu ambao tumewarithisha mfumo uleule wa umasikini. Inatakiwa tubadilike, tusijirahisishe kwa kukimbilia kuajiliwa. Kwa hakika maisha tunayoishi ni ya kufuata mkumbo ati kwasababu Fulani kafanya hivi basi na wewe unataka kufanya vivyo hivyo.
       Kuna dhahabu kila mahali lakini watu hawajafundishwa namna ya kuziona. Mtu wa kawaida atakwenda kila mahali mgodini lakini hawezi kuziona dhahabu. Je wewe unataka kuziona dhahabu?
Basi fuatana nami ili tujue jinsi ya kutumia na kuendeleza vipaji alivyotupa mungu badala ya kutegemea hilizi na kuuwa binadamu wenzetu kwa minajili ya kupata utajili.

1: Je Una sababu?

      Una nia ile kutoka moyoni? Watu wengi sana wanapenda kuwa matajiri na kujikwamua kiuchumi, lakini hawana nia ile ya kweli. Barabara ya kuuelekea utajiri kwao imekuwa ni ndefu mno na milima ya kupanda ni mingi mno, hivyo kujikuta wakikata tamaa na kuona ni bora kurejea katika hali ya awali.
     Kuwa na sababu, dhumuni na uhitaji na sio kusema sihitaji na hata ukiulizwa kwa nini unataka kuwa tajiri ni lazima uwe na sababu. Je unahitaji kufanya kazi maisha yako yote, je unahitaji kuajiliwa na kulazimishwa kufanya hata yale usiyotaka, unataka kufa na kuacha familia yako masikini. Najua wengi majibu yetu ni sio, lakini je tuna ile nia ya kutoka moyoni ya kusema hapana kwa maswali hayo hapo juu.
    Nadhani hatimaye tukifanya kazi kwa uaminifu na kupata kipato cha kutufanya tuwe matajiri tuna weza, kuzunguka katika dunia hii na kuishi maisha tunayoyataka, tutakuwa huru kumiliki muda na maisha yetu na hatimaye hatutakuwa watumwa wa pesa bali pesa ndio itakuwa mtumwa wetu.
     Siwezi kuacha kusema tena “unatakiwa uwe na sababu na nia kwa nini unataka kuwa tajiri??” Haya safari kuelekea utajiri ni ndefu sana na waweza kurudi nyuma sana wakati mwingine, lakini kama una ile nia ya kweli utasimama tena na kusonga mbele. Waingereza wana msemo wao “life starts at 40”. Huu ni ujumbe kwa vijana kabla ya kufikisha miaka 40 unatakiwa uwe umetengeneza maisha yako uwe huru kiuchumi.
Je kupata utajiri ni rahisi?. Sio rahisi na wala sio vigumu pia lakini ukweli ni kwamba bila kuwa na sababu, nia na dhumuni kila kitu ni kigumu katika maisha.

No comments:

Post a Comment