Wiki nzima tumekuwa tukitengeneza documentary ambayo
itatumika katika matangazo ya kutangaza bidhaa zitokanazo na kakao. Matangazo
hayo yanatengenezwa na UNILIVER kupitia
kitengo chao cha utengenezaji wa chocolate cha MAGNUM.
Matangazo hayo yataonyeshwa katika nchi za ulaya hasa zenye
walaji wa bidhaa za chocolate. Shukrani za zati ziende kwa kampuni ya BIOLANDS
Kyela kwa kufanikisha ujio huo.
Ni matumaini yetu kwamba baada ya matangazo hayo kuanza
kurushwa huko ulaya itaongeza walaji wa bidhaa za kakao na hivyo kufanya zao
hilo kuwa na bei nzuri kwa wakulima nahatimae waweze kupata premium kwa mazao
yao.
Hata mimi mwana blog mwenzako nilipata nafasi ya kukutana na
wageni kutoka nchi za ulaya kama vile Sweden na Uingereza, na kizuri zaidi
nimealikwa niende kutembelea nchi zote walikotoka hao na kwamba watakuwa
wenyeji wangu,,,wana blog je nauri hizo nitatoa wapi??.
Hapa chini nawapa vionjo muweze kuona baadhi ya picha
tulizopiga nitaendelea kuwatupia kidogo kidogo siku hadi siku.
Na pia ni fursa sasa kwa wakulima wa kakao kuongeza
uzalishaji wa kakao na iliyo bora, kwa kuwa sasa hivi kutokana na ushindani wa
kibiashara watu wameacha kabisa kufuata kanuni bora za kilimo. Jamani tuachane
na ujinga huo hebu tuelimike na tujue kuwa kakao ni chakula na hivyo tufuate
kanuni bora za kilimo tuache kuwatumia wafanyabiashara waitwao njemke hao kwa
hakika baada ya muda watkuja kuharibu zao la kakao.
HEBU TIZAMA PICHA HIZI HAPA CHINI.
Ni asubuhi katika milima ya Livingstone tukianza
maandalizi ya shooting.
Mti wa kakao ukiwa na matunda.
Wadau wa zao la kakao hao Bw. Ephraem Mwandambo ( katikati
), Expeditor Nzalalila ( kushoto ) na Frank Samwel ( kulia ) wakiwa katika shamba darasa la kakao. Hawa jamaa ni shiiida katika zao la
kakao yaani wamebobea.

This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteAsante sana, nilikuwa natafuta sana taarifa hii sasa nimeipata
ReplyDelete