Monday, 17 November 2014

TUMAINI KWA WAKULIMA WA KAKAO (COCOA)

 Kakao ni zao linalotumika kutengeneza vitu vitamu sana kama chocolate na ice cream. Ni zao ambalo kwa Tanzania linastawi sana katika mikoa ya Mbeya wilayani Kyela, Busokelo na Ileje na katika mkoa wa Morogoro.
Wiki nzima tumekuwa tukitengeneza documentary ambayo itatumika katika matangazo ya kutangaza bidhaa zitokanazo na kakao. Matangazo hayo yanatengenezwa na UNILIVER  kupitia kitengo chao cha utengenezaji wa chocolate cha MAGNUM.
Matangazo hayo yataonyeshwa katika nchi za ulaya hasa zenye walaji wa bidhaa za chocolate. Shukrani za zati ziende kwa kampuni ya BIOLANDS Kyela kwa kufanikisha ujio huo.
Ni matumaini yetu kwamba baada ya matangazo hayo kuanza kurushwa huko ulaya itaongeza walaji wa bidhaa za kakao na hivyo kufanya zao hilo kuwa na bei nzuri kwa wakulima nahatimae waweze kupata premium kwa mazao yao.
Hata mimi mwana blog mwenzako nilipata nafasi ya kukutana na wageni kutoka nchi za ulaya kama vile Sweden na Uingereza, na kizuri zaidi nimealikwa niende kutembelea nchi zote walikotoka hao na kwamba watakuwa wenyeji wangu,,,wana blog je nauri hizo nitatoa wapi??.
Hapa chini nawapa vionjo muweze kuona baadhi ya picha tulizopiga nitaendelea kuwatupia kidogo kidogo siku hadi siku.
Na pia ni fursa sasa kwa wakulima wa kakao kuongeza uzalishaji wa kakao na iliyo bora, kwa kuwa sasa hivi kutokana na ushindani wa kibiashara watu wameacha kabisa kufuata kanuni bora za kilimo. Jamani tuachane na ujinga huo hebu tuelimike na tujue kuwa kakao ni chakula na hivyo tufuate kanuni bora za kilimo tuache kuwatumia wafanyabiashara waitwao njemke hao kwa hakika baada ya muda watkuja kuharibu zao la kakao.

HEBU TIZAMA PICHA HIZI HAPA CHINI.
Ni asubuhi katika milima ya Livingstone tukianza maandalizi ya shooting.





Mti wa kakao ukiwa na matunda.



Shooting inaendelea katika ofisi za BIOLANDS Kyela ikionyesha kakao inavyochambuliwa.


Kakao ikiwa imeanikwa katika ofisi za BIOLANDS Kyela ili kufikia unyevu unaotakiwa.



Wadau wa zao la kakao hao Bw. Ephraem Mwandambo ( katikati ), Expeditor Nzalalila ( kushoto ) na Frank Samwel ( kulia )  wakiwa katika shamba darasa  la kakao. Hawa jamaa ni shiiida katika zao la kakao yaani wamebobea.



ikianikwa juu ya vichanja katika usafi wa hali ya juu ili kuhakikisha ubora unadhibitiwa



2 comments:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Asante sana, nilikuwa natafuta sana taarifa hii sasa nimeipata

    ReplyDelete